Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, amehojiwa kwa saa sita na baadaye kulazwa rumande na Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.Mbunge huyo ambaye jana mchana alikamatwa na polisi nyumbani kwake baada ya kuizunguka kwa saa kadhaa, anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea Februari 27, mwaka huu kwenye ukumbi wa Karemjee baada ya uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam kuahirishwa kwa kile kilichoelezwa ni kutokana na zuio la mahakama.Mbali na Mdee, watu wengine watatu wakiwamo
Diwani wa Kata ya Saranga, Efraim Kinyafu na Diwani wa Kata ya Mbezi, Hamfrey Sambo wote wa Chadema na kada wa chama hicho kata ya Mabibo, Shafii Juma, wanashikiliwa na polisi kuhusiana na vurugu hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni