Jumanne, 1 Machi 2016

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) YA TOA ONYO KWA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI



























Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevipa onyo na kuvipiga faini vituo viwili vya redio kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.Vituo hivyo ni Entertainment FM (E FM) cha Dar es Salaam na Kahama FM Stereo ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Akitoa maamuzi yaliyofikiwa na Kamati ya Maandili ya TCRA, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margaret Munyagi, alisema vituo hivyo vimebainika kukiuka sheria na kanuni za utangazaji.

Amevitaka vewe na usimamizi mzuri wa vipindi vyao.
Munyagi alisema kamati yake imekipa onyo kali na faini ya sh milioni moja kituo cha Efm na endapo kitarudia, hatua kali zaidi zitachukuliwa.Alisema Januari 4 mwaka huu, kituo hicho katika kipindi cha ‘Joto la Asubuhi’ katika kipengele cha ‘Sala ya Siku’, kilichorushwa kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi, Mtangazaji alihamasisha vitendo vya wizi, ngono na uchochezi wa kidini.
Katika utetezi wake, Mkurugenzi wa kituo hicho, Dennis Busulwa pamoja na kukiri kufanya kosa, alisema kituo chake kilijibebesha mzigo mzito wakati bado ni wachanga katika utangazaji na kutokana na kosa hilo waliamua kukiondoa kipengele hicho.

Hakuna maoni: