Meneja wa
Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani
ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika Manispaa ya
Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin, (katikati)
na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya Go4school, Henning
Nathow.
Katika kusaidia
kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi jijini
Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na Alliance
Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada wa elimu
na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika Manispaa ya
Ilala, Dar es Salaam.
Akizungumzia msaada
huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa lengo la
kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao wengi
wao wamekuwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuvuka barabara.
Alivitaja vifaa
hivyo kuwa ni alama za barabarani ambazo zinaonyesha alama za
kusimamisha magari ili wanafunzi wavuke, makoti yanayowatambulisha
waongozaji, kofia za kuwazuia na jua na mipira ya michezo mashuleni na
watatoa elimu katika shule hizo ili kuwasaidia watoto kujua sheria za
barabarani.
“Tumeamua kutoa
msaada huu kwa shule 18 na tutatoa elimu na tutakabidhi vifaa …
tunaamini msaada huu utaweza kuwasaidia watoto hao na tunaamini
itasaidia kupunguza ajali barabarani,” alisema Bi. Tharaia.
Akipokea vifaa
hiyvo kwa niaba ya Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter alisema
wanaishukuru CFAO Motors Group kwa kutambua umuhimu wa elimu na kutoa
vifaa vitakavyoweza kusaidia kuongoza wanafunzi wavukapo barabara.
"Tunashukuru sana
kwa msaada huu na mmeonyesha ni jinsi gani mnatambua umuhimu wa elimu na
sisi tupo pamoja nanyi na tupo tayari kupokea elimu hiyo," alisema Bi.
Helen.
Alizitaja baadhi ya
shule ambazo zitapata vifaa hivyo kuwa ni Shule ya Msingi Msimbazi,
Boma, Mnazi Mmoja, Uhuru Mchanganyiko, Tabata, Ilala, Lumumba,
Muhimbili, Buguruni, Kasulu, Mkoani, Msimbazi Mseto, Hekima, Amana,
Mtendeni, Buguruni Viziwi na Tabata Jeta na Mtandani.
Pamoja na hayo pia
kunataraji kufanyika mashindano ya mbio za magari yaliyo na lengo la
kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na kampuni ya CFAO Motors
Group yanayofanyika nchini na yanataraji kumalizikia nchini Rwanda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni