Dunia
nzima nadhani inamfahamu Lucky Dube ambaye ni mwanamuziki nguli wa
reggae kutoka Afrika Kusini, ambaye tungo zake zimeweka rekodi kubwa
kwenye muziki huo mpaka sasa anapotimiza miaka 9 tangu kuuawa kwake,
baada ya kupigwa risasi na watu ambao walitaka kumuibia gari lake
alipoenda kuwashusha watoto wake kwa mjomba wao.
Lucky Philip Dube alizaliwa tarehe 3 August 1964 katika eneo la Ermelo kwa sasa linajulikana kama Mpumalanga nchini Afrika Kusini akiwa ni mtoto wa kwanza kwa mama yake. Wazazi wa Lucky Dube walitengana kabla hajazaliwa, na tetesi zinasema kuwa baba yake alikuwa ni raia wa Zimbabwe, na kabla Lucky hajazaliwa alilazimika kuondoka na kurudi Zimbabwe.