Mwanariadha mlemavu wa Afrika
Kusini Oscar Pistorius amenyimwa ruhusa ya kukata rufaa uamuzi wa
mahakama wa kumpata na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Mahakama ya Kikatiba ndiyo iliyotoa uamuzi huo, na ina maana sasa kwamba Pistorius atahukumiwa Aprili.Pistorius alimuua Bi Steenkamp Februari 2013 baada ya kufyatua risasi mara nne kupitia mlango wa choo alimokuwa mpenzi huyo wake.
Uamuzi wa awali wa kumpata na kosa la kua bila kukusudia ulibatilishwa Desemba mwaka jana na badala yake majaji wakampata na hatia ya mauaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni