Baraza la mitihani
Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nnewamwaka2015
yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
Akitangaza matokeo hayo,
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesemakuwa jumla
watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihaniwa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 amba ufaulu
ulikuwa 68.33%.
Msonde amesema kwa
upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia
67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana
wakiwa 124,871 (71.09).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni